Pata taarifa kuu
MALTA-ITALIA

Boti nyingine iliyobeba wahamiaji haramu yazama katika bahari ya Mediterranean na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30

Boti iliyobeba wahamiaji takribani mia mbili imezama katika bahari ya Mediterranean na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 katika kisiwa cha Malta, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa jeshi la uokoaji la Italia na shirika la habari la nchi hiyo.

http://www.stuff.co.nz
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo linakuja takribani juma moja baada ya boti nyingine iliyokuwa na wahamiaji haramu kutoka barani Afrika kuzama na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 300 karibu na visiwa vya Lampedusa Kusini mwa Italia.

Boti hiyo imezama umbali wa takribani kilometa 120 kutoka Lampedusa na takribani kilometa 110 kutoka Malta.

Serikali ya Malta na Italia wanashirikiana kufanikisha zoezi la uokoaji na inaelezwa kuwa helikopta na meli zimekuwa zikitumika kuwabeba manusura wa ajali hiyo ili kuwafikisha katika eneo la nchi kavu.

Kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, wahamiaji 32,000 wamewasili Kusini mwa Italia na Malta mwaka huu na tayari theluthi mbili wameomba kupewa uraia.

Wahamiaji wengi zaidi waliowasili mwaka huu wamekuwa wakikimbia machafuko yanayoendelea nchini Syria na wengine wametokea katika mataifa ya Kaskazini mwa Africa.

Takwimu zaidi zinakadiria kuwa wahamiaji kati ya 17,000 na 20,000 wamekufa maji katika kipindi cha miaka 20 iliyopita wakiwa kwenye harakati za kuingiz barani Ulaya kwa lengo la kutafuta hifadhi na maisha bora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.