rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ban Ki Moon Eritrea Italia Somalia UN Angelino Alfano

Imechapishwa • Imehaririwa

Wahamiaji Haramu kutoka Barani Arika wapatao 300 wanatajwa kupoteza maisha kwenye ajali ya boti huko Italia

media
Miili ya wahamiaji haramu waliopoteza maisha kwenye ajali ya meli katika Kisiwa cha Lampedusa REUTERS/Antonio Parrinello

Wahamiaji haramu wapatao mia tatu kutoka Barani Afrika hasa mataifa ya Eritrea na Somalia wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kushika moto na kisha kuzama ikiwa na watu wanaofikiwa mia tano.


Hofu ya idadi ya watu waliopoteza maisha imeongezeka kutokana na kupatikana kwa manusura mia moja hamsini pekee baada ya Waokoaji kufanya zoezi hilo kwa zaidi ya saa ishirini la kusaka abiria waliokuwa wanasafiri na boti hiyo.

Wavuvi na Kikosi Malum cha Uokozi ambao wamekuwa katika operesheni ya kuwaokoa wahamiaji haramu wamesema zoezi lilikuwa gumu sana kutokana na Bahari kuchafuka karibu kabisa na Kisiwa cha Lampedusa.

Zoezi la kusaka miili ya wahamiaji haramu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo zingali zinaendelea kwa kutumia boti ziendazo kasi pamoja na helkopta lengo likiwa ni kujua idadi kamili ya watu waliopoteza maisha.

Umoja wa Mataifa UN umeeleza kuguswa mno na tukio hilo na kusema wakati umefika sasa wa kuhakikisha harakati za wahamiaji haramu zinadhibitiwa ili kuepusha majanga yanayoendelea kushuhudiwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amesema wakati wa kumaliza majanga ya kuzama kwa meli na kuchangia vifo vya wahamiaji haramu umefika na kila juhudi zinafaa kuchukuliwa.

Mapema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Angelino Alfano aliwaambia wanahabari miili tisini na tatu ilipatikana wakiwemo watoto watatu na wanawake wawili wajawazito kabla ya baadaye kusema miili mingine zaidi ya arobaini imeonekana ikielea Baharini.

Wahamiaji haramu kutoka nchi za Somalia, Eritrea na Ghana wakiwa njiani kueleka nchini Italia kujipatia hifadhi walipata ajali baada ya boti yao kushika moto na kisha kuzama kitu kilichochangia vifo vya abiria walioamua kujitosa baharini.