rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Omar Al Bashir Sudani Mashood Adebayo Baderin

Imechapishwa • Imehaririwa

Serikali ya Sudan yanyoshewa kidole cha lawama kutokana na kutumia nguvu kubwa kukabiliana na maandamano

media
Waandamanaji nchini Sudan wakipinga kupanda kwa ruzuku kwenye bei ya mafuta

Serikali ya Sudan imeendelea kukabiliwa na lawama kutokana na namna ambavyo inashughulikia maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta kulikosababishwa na kuongezwa kwa ruzuku kwenye bidhaa hiyo muhimu.


Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu limenyoosha kidole cha lawama kwa Serikali ya Sudan likisema imekuwa ikitumia nguvu kubwa kukabiliana na Waandamanaji bila ya kujali haki zao msingi.

Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu Mashood Adebayo Baderin amesema uchunguzi wao wa awali umeonesha serikali ya Khartoum imekuwa aiheshimu kabisa haki za binadamu.

Baderin ameongeza miongoni mwa vitendo vinavyoidhinisha hilo ni hatua ya Jeshi la Polisi kuwafyatulia risasi za moto waandamanaji ambao wanahaki ya kupaza sauti zao kwa njia hiyo.

Mratibu huyo wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu amesema hatua hiyo ya kutumia risasi za moto kuwasambaza waandamanaji imechangia watu wengi kupoteza maisha japokuwa serikali imekuwa ikitoa takwimu za chini.

Shirika hilo limeitaka Serikali ya Rais Omar Hassan Ahmed Al Bashir kuheshimu haki ya msingi ya watu kuandamana kwa amani badala ya kutumia nguvu kuwanyamazisha wakati wana madai yao ya msingi.

Baderin kwa upande wake amesema wakati umefika kwa Serikali na waandamanaji kurejea kwenye meza ya mazungumzo kwa lengo la kupata suluhu juu ya kupanda kwa bei hiyo ya mafuta ili nchi hiyo irejee kama ilivyokuwa awali.

Mapema juma hili Rais Al Bashiri alizungumza na wanahabari na kushusha lawama nzito kwa waaandamanaji aliowatuhumu kutumiwa na wapinzani kwa lengo la kulemaza shughuli za ukuaji wa uchumi.

Serikali ya Khartoum imejiapiza kuendelea na mchakato wake wa kuhakikisha tozo iliyoongezwa kwenye mafuta na kuchangia bei ya bidhaa hiyo kupanda haitaondolewa kwani ina lengo la kuhakikisha uchumi unakuwa haraka.

Waandamanaji wapatao mia saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kufanya maandamano yaliyochangia madhara makubwa yakiwemo kuchomwa moto kwa vituo vya mafuta, magari na kuharibiwa kwa maduka.