Pata taarifa kuu
Sierra Leone

Rufaa ya Taylor yatupiliwa mbali, ahukumiwa miaka 50 kama ilivyoamriwa hapo awali

Mahakimu katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huko Hague Uholanzi wamemhukumu rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor kifungo cha miaka hamsini jela kwa kukutwa na hatia ya kufadhili waasi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone. 

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor africvilla.com
Matangazo ya kibiashara

Hapo awali mnamo April 26 mwaka 2012 mahakama maalumu nchini Sierra Leone ilimkuta Taylor (65)na hatia ya makosa 11 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo ugaidi, uuaji , ubakaji na kutumia watoto wadogo katika jeshi na hivyo kuhukumiwa miaka 50 jela.

Mahakimu katika mahakama maalumu nchini Sierra Leone SCSL leo Alhamisi wamekataa rufaa ya Taylor dhidi ya hukumu yake ya awali.

Mkurugenzi wa haki katika shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch Elise Keppler amesema kuwa uamuzi wa majaji hii leo dhidi ya Taylor unaweka alama muhimu kwamba hata wake watu walioko kwenye madaraka ya juu wanaweza kuwajibishwa.

Aidha Elise amesisitiza kuwa Kesi ya Taylor na kazi iliyofanywa na mahakama maalumu ya Sierra Leone kwa pamoja vimechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa haki baada ya makosa ya ukatili yaliyotekelezwa wakati wa mapigano nchini Sierra Leone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.