Pata taarifa kuu
INDIA-MAOIST

Singh: Tutahakikisha tunapambana na waasi wa Maoist

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh ameagiza vyombo vya usalama nchini humo kuhakikisha inawasaka wapoganaji wa kundi la waasi wa Maost ambao wametekeleza mauaji ya watu 24 wakiwemo baadhi ya wabunge.

Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh mwenye vazi jeupe akiwa na mbunge wa bunge la Congres, Sonia Gandhi wakiwatembelea wabunge waliojeruhiwa
Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh mwenye vazi jeupe akiwa na mbunge wa bunge la Congres, Sonia Gandhi wakiwatembelea wabunge waliojeruhiwa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetekelezwa kwenye eneo la mji wa Raipur ambapo wabunge hao nawafuasi wao walivamiwa na kundi la wapiganaji wenye silaha na kuanza kushambulia msafara wao na kisha kutokomea maeneo ya msituni.

Sahambulio hili ni baya zaidi kuwahi kutekelezwa na wapiganaji waasi wa kundi la Maost ambao wamekuwa wakipigana na Serikali ya India kwa miongoz kadhaa wakidai haki sawa miongoni mwa jamii yao.

Serikali imekiri kuwa shambulio hili ni baya zaidi kutekelezwa na waasi wa Maoist katika kipindi cha miaka mitatu toka Serikali iimarishe usalama kwenye eneo hilo.

Mkuu wa bunge la Congress, Sonia Gandhi amefika kwenye eneo la tukio akiambatana na waziri mkuu Manmohan Singh ambapo kwa pamoja wamelaani shambulio hilo na kuapa kukabiliana na waasi hao.

Wapiganaji wa kundi la Maoist wamekuwa wakipigana na vikosi vya Serikali kwenye mji wa Raipur ambapo wamekuwa wakidai kupewa ardhi na Serikali pamoja na kuishinikiza Serikali kupeleka maendeleo kwenye jimbo hilo.

Nand Kumar Patel na mtoto wake aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, Mahendra Karma ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulio hilo ambapo walishiriki kuandaa mpango mkakati wa kukabiliana na wapiganaji wa Maoist mwaka 2005.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.