Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani yasema bado haijaamua kupeleka wanajeshi wake nchini Syria

Rais wa Marekani Barack Obama amesema hawezi kuweka bayana iwapo Taifa lake litapeleka wanajeshi wake Syria kukabiliana na majeshi ya Rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad. Akiwa ziarani Costa Rica Rais Obama amewaambia waandishi wa habari kuwa bado hajaona iwapo hatua ya kupeleka wanajeshi wake Syria itakuwa na faida kwa nchi hizo.

REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwapo na taarifa kuwa huenda utawala wa Obama ukaangalia uwezekano upya wa kuwafadhili waasi wa Syria kwa silaha baada ya kuwepo kwa tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya raia.

Akizungumzia suala hilo, Obama amesema wanajua kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika ingawa hawana uthibitisho wa kutosha hivyo wanasubiri uchunguzi zaidi ili kubaini ni lini, wapi na jinsi gani silaha hizo zimekuwa zikitumiwa.

Marekani inaangalia uwezekano wa kuwalinda raia wa Syria wakati wakisubiri uthibitisho wa matumizi ya silaha hizo katika mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa UN mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu sabini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.