Pata taarifa kuu
INDIA

Jeshi la Polisi nchini India limekiri kupewa mapema taarifa za uwepo wa mpango wa mashambulizi huko Hyderabad

Jeshi la Polisi nchini India limesema Wanamgambo wa Kiislam walishatoa onyo la kuwa na mapngo wa kutekeleza shambulizi katika eneo la Hyderabad lakini hakuna taadhari zozote ambazo zilichukuliwa tangu awali. Jeshi la Polisi linasema baada ya kutolewa kwa tishio hilo na Wanamgambo wa Kundi moja la Mujahideen waliwakamata wafuasi wawili wa kundi hilo na kuwahoji na kueleza mpango wao wa kufanya mashambulizi Delhi, Mumbai, Hyderabad na Pune.

Askari nchini India wakiwa kwenye doria baada ya kutokea kwa shambulizi nje ya Ukumbi wa Sinema huko Hyderabad
Askari nchini India wakiwa kwenye doria baada ya kutokea kwa shambulizi nje ya Ukumbi wa Sinema huko Hyderabad
Matangazo ya kibiashara

Kamishna wa Polisi katika Mji wa Delhi Shri N. Shrivastava amesema kama hatua madhubuti zingechukuliwa ni wazi kabisa mashambulizi mawili yaliyotekelezwa Hyderabad na kusababisha vifo vya watu 14.

Mashambulizi hayo mawili yametekelezwa katika eneo la Dilsukh Nagar na kuongeza hofu ya usalama katika nchi ya India baada ya kutokea kwa mashambulizi hayo yanayotajwa kutekelezwa na Wapiganaji wa Kundi la Mujahideen.

Mashambulizi haya ya mabomu ni ya kwanza nchini India tangu mara ya mwisho kutokea kwa tukio kama hilo mwaka 2011 na sasa ulinzi zaidi umeendelea kuimarisha ili kudhibiti hatari yoyote.

Tukio hilo la mashambulizi katika Mji wa Hyderabad limesababisha vifo na majeruhi ya watu wengi ambao ni vibarua waliokuwa wakitafuta chakula kwenye soko la matunda na kisha waelekee nyumbani.

Serikali ya India imeanza msako madhubuti kuwabaini wale wote ambao wamehusika kwenye mashambulizi hayo ya mabomu na kuchangia vifo vya watu 14 na kujeruhi wengine kadhaa.

Waziri Mkuu Manmohan Singh amesema Jeshi la Polisi halitalala katika kuhakikisha wanawasaka wafuasi wa Mujahideen ambao wanatajwa kuhusika kwenye kupanga na kutekeleza mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo mawili yametekelezwa katika kituo cha basi na jingine likiwa nje ya ukumbi wa sinema na tayari wachunguzi wameanza kukusanya mabaki ya bomu hiyo kujua ni la aina gani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.