rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Al Qaeda Osama Bin Laden Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Mtuhumiwa wa ugaidi Abu Qatada ashinda rufaa yake Uingereza

media
REUTERS/Stefan Wermuth/Files

Mtuhumiwa wa masuala ya Ugaidi na pia anayetajwa kuwa alikuwa mshirika wa karibu wa kiongozi wa mtandao wa kigaidi duniani Al-Qaeda, Marehemu Osama Bin Laden, Abu Qatada, ameshinda rufaa yake dhidi ya serikali ya Uingereza kutaka ahamishiwe nchini Jordan.


Mahakama kuu nchini Uingereza imetupilia mbali madai yote ya serikali ya Uingereza na kudai kuwa iwapo mtuhumiwa huyo atarejeshwa nchini Jordan kusikiliza kesi zinazomkabili huenda asitendewe haki.

Uamuzi wa mahakama hiyo mekuwa pigo kwa serikali ya Uingereza mabayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikijaribu kuhakikisha mtuhumiwa huyo anarejeshwa nchini Jordan.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Theresa May amesisitiza serikali kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na kuongeza kuwa bado wana amini Abu Qatada ni hatari kwa usalama wa nchi.

Abu Qatada alihukumiwa nchini Jordan mwaka 1998 kwa tuhuma za kushirikiana na magaidi hukumu ambayo wakati ikitolewa hakuwepo nchini Jordan.