Pata taarifa kuu
MAREKANI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laendelea kugawanyika kuhusu kumaliza mzozo wa Syria

Nchi za Marekani na Urusi zimeendelea kuvutana kuhusu namna ya kumaliza mzozo wa machafuko nchini Syria huku kila upande ukimshutumu mwenzake kwakuendelea kusababisha umwagikaji damu nchini humo.

Hillary Clinton (kushoto) waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Sergey Lavrov (katikati) waziri wa mambo ya nje wa Urusi wakizungumza na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon (Kulia)
Hillary Clinton (kushoto) waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Sergey Lavrov (katikati) waziri wa mambo ya nje wa Urusi wakizungumza na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon (Kulia) UN Photo/Devra Berkowitz
Matangazo ya kibiashara

Mvutano huo ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umeendelea kudhihirisha mgawanyiko mkubwa ulioko baina ya mataifa yenye kura za turufu kwenye Umoja huo kuhusu kumaliza machafuko nchini humo.

Kwenye kikao cha siku ya Jumatano waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton ameyashutumu mataifa ambayo yanaunga mkono utawala wa rais Bashar al-Asad akisema kuwa na zenyewe ni miongoni mwa magaidi ambao wanauwa watu wao wenyewe.

Waziri Clinton ametoa maneno hayo akiinyoshea kidole nchi ya Urusi na Uchina ambazo zimekuwa mstari wa mbele kukataa uvamizi wowote wa kijeshi dhidi ya taifa la Syria.

Wakati Marekani ikiishutumu Urusi kwa kuendelea kumsaidia Asad na utawala wake kuendeleza mauaji nchini mwake, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov kwa upande wake ameishutumu nchi ya Marekani kwa kuendelea kufadhili ugaidi duniani.

Lavrov ametolea mfano hatua ya Marekani kuendelea kuwafadhili kwa silaha waasi wanaopigana na serikali ya Syria na kuongeza kuwa kitendo hicho ni wazi kinafadhili ugaidi kwa makundi hayo kuendeleza uasi dhidi ya raia.

Licha ya kushutumiwa na Marekani, waziri wa mambo ya nje wa Urusi ameendelea kusisitiza msimamo wa nchi yake kuhusu Syria na kwamba haitafanya mabadiliko yoyote kuhusu hatua za kuchukua kumaliza machafuko nchini humo.

Lavrov ameongeza kuwa suala la kumaliza machafuko nchini humo liko mikonono mwa nchi ya Syria na hasa waasi ambao wamekataa katu kuweka silaha chini kuruhusu mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.