Pata taarifa kuu
INDIA

Wafanyakazi nchini India wafanya mgomo wa nchi nzima kushinikiza mabadiliko ili kukuza uchumi

Vyama vya Upinzani nchini India pamoja na Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi wameanza mgomo wa nchi nzima kushinikiza mabadiliko kwenye sekta ya biashara ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Wafanyakazi wa sekta mbalimbali nchini India wakiwa kwenye mgomo na kusababisha kuzuia njia za reli
Wafanyakazi wa sekta mbalimbali nchini India wakiwa kwenye mgomo na kusababisha kuzuia njia za reli
Matangazo ya kibiashara

Chama Kikuu Cha Upinzani Cha BJP kimeungana na vyama vingine vidogo kwenye mgomo huo ambao unapinga ongezeko la ruzuku ya asilimia kumi na nne kwenye bei ya nishati ya mafuta.

Shule, maduka na ofisi za serikali zimefungwa kutokana na mgomo huo ambao umelemaza shughuli nyingi katika nchi na India iliyoshuhudioa wafuasi wengi wa Chama cha Bharatiya Janata wakishiriki.

Maelfu ya askari wamepelekwa katika Jiji la Kolkata uliopo Magharibi mwa Jimbo la Bengal kudhibiti machafuko ambayo yanaweza kutokea na kulenga maduka, masoko na ofisi.

Shughuli zimelazimika kusimama kwa kipindi cha saa ishirini na nne kwa ajili ya kutathmini mgomo huo utakuwa na madhara gani hasa kwa uchumi wa taifa hilo ambao umezidi kuwa mashakani.

Mgomo huu umeiweka pabaya serikali ya Waziri Mkuu Manmohan Singh ambayo siku ya jumanne ilishuhudia uhusiano wake na chama walichounda serikali pamoja kikijitoa kutokana na tofauti za kimsimamo.

Waandamanaji hao wamejiapiza kufanya maandamano yao hadi pale ambapo serikali itakapokuwa tayari kushughulikia matatizo yaliyopo ili yaweze kusaidia ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.

Taarifa za uhakikia kutoka ndani ya Shirika la reli nhini humo limethibitisha safari zake kuathirika kutokana na wafanyakazi hao kujitokeza mitaani na kuzuia njia za garimoshi linalotumika kusafirishia abiria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.