Pata taarifa kuu
MISRI

Wakati raisi mteule wa misri akitarajia kuapishwa,taasisi ya fedha ya kimataifa yaahidi kuiwezesha Misri

Mkuu wa taasisi ya fedha ya kimataifa Christine Lagarde amemuarifu raisi mpya wa serikali ya kiraia nchini Misri mohamed Morsi kuwa taasisi ya fedha ipo tayari kuisaidia Misri kifedha.

Raisi mpya wa Misri ambaye anatarajia kula kiapo leo nchini humo,Mohammed Morsi
Raisi mpya wa Misri ambaye anatarajia kula kiapo leo nchini humo,Mohammed Morsi REUTERS/Egypt TV
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa taasisi ya fedha ya kimataifa alisema hayo kwa niaba ya mkuu huyo na kumpongeza raisi Morsi kwa kuchaguliwa jambo linaloielekeza Misri katika hatua muhimu ya mpito.

Taasisi hiyo ya fedha imejipanga kuiwezesha misri baada ya kujadili hali ya kiuchumi ya nchi hiyo na jitihada za taasisi ya fedha katika kuinua uchumi wa Misri kwa siku zijazo ambapo Lagarde ameahidi kufanya kazi sambamba na mamlaka hiyo mpya iliyowekwa madarakani na raia.

Aidha hii leo wamisri wanatarajia kushuhudia kuapishwa kwa raisi wao mpya mohamed Morsi ambaye ataapishwa katika mahakama ya kikatiba mara baaada ya kuwepo kwa tofauti na jeshi la nchi hiyo kuhusu kuyaachia madaraka kwa utawala wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.