Pata taarifa kuu
OSLO-NORWAY

Upande wa utetezi wataka Breivik ahukumiwe kama mtu mwenye akili timamu

Mawakili wanaomtetea mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 na kujeruhi wengine zaidi ya 200 kwenye mji wa Oslo nchini Norway, Anders Breivik wameiomba mahakama kuu inayosikiliza kesi hiyo kumchukulia mteja wao kama mtu wenye akili timamu.

Anders Behring Breivik mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway akiwa mahakamani mjini Oslo
Anders Behring Breivik mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway akiwa mahakamani mjini Oslo REUTERS/Berit Roald/NTB
Matangazo ya kibiashara

Mawakili hao wameyasema hayo wakati wakihitimisha utetezi wao, na kudai kuwa kwakuwa Brivik mwenyewe amekiri kutekeleza mauaji hayo kwa malengo, mteja wao alitenda kosa hilo akiwa na akili timamu na kwamba hata sasa ana akili timamu.

Ombi la upande wa utetezi linakuja kufuatia upande wa mashtaka kuitaka mahakama hiyo kumtangaza Breivik kama mtue asiyekuwa na akili timamu na kutaka apelekwe kwenye kitengo maalumu cha wagonjwa wa akili.

wakitoa hitimisho lao kwenye kesi hiyo mjini Oslo, upande wa mashtaka umedai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo bila ya kujitambua na kwamba hafahamu alichokuwa anakitenda na kutaka awekwe kwenye uangalizi maalumu.

Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kutoa hitimisho lake kwenye utetezi wake wa mwisho kabla ya majaji wanaosikiliza kesi hiyo kutoa uamuzi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.