Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UGIRIKI

Viongozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya EU wakubaliana kuisadia Ugiriki kuondokana na madeni

Viongozi kutoka Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya EU ambao wamekutana kwenye mkutano wa dharura nchini Ubelgiji katika Jiji la Brussels wamekubaliana kwa kauli moja kuiunga mkono Ugiriki ambayo inakabiliwa na hali mbaya ya madeni iliyochangiwa na kutetereka kwa uchumi wake.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao baada ya mjadala mkali huko Brussels wameafikiana kuondoa asilimia hamsini ya deni ambalo Ugiriki inadaiwa huku Ukanda huo wa Ulaya ukiongeza mfuko wake wa madeni na kukusanya jumla ya euro trilioni moja kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo ya kukabiliana na madeni.

Mkutano huo ambao ulimaliza usiku wa maneno kutokana na uwepo wa mvutano mkali baina ya viongozi hao ulitamatishwa kwa agizo lililotolewa kwa Benki zilizochini ya Umoja wa Ulaya kuhakikisha wanachukua jukumu la kulipa deni la Ugiriki kwa asilimia hamsini.

Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreou ni mmoja wa wale ambao wamepokea kwa mikono miwili uamuzi huo wa EU na kusema umechangia uwepo wa siku mpya si kwa nchi yake pekee bali hata kwa Ukanda wote wa Ulaya ambao umejawa na hofu ya kutetereka kwa uchumi wake.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Nicolas Srakozy ndiyo walikuwa vinara wa kuhakikisha nchi za Umoja wa Ulaya EU zinachukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo la madeni ambalo linaikumba Ugiriki na kuleta hofu ya kusambaa kwenye nchi za Italia na Uhispania.

Baada ya kufikiwa makubaliano hayo Rais Sarkozy amesema pongeza hatua hiyo na kuanisha huu ni mwanzo wa kuweza kukabiliana na janga la madeni ambalo linahofiwa kuweza kutikisa uchumi wa mataifa mengi ya Ulaya katika siku za usoni.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye ni mmoja wa wapatanishi kwenye mgogoro huo wa madeni amenukuliwa akisema anafikiri muafaka uliofikiwa utasaidia kufikiwa kwa matarajio ya kuimarisha uchumi yalitokuwa yamekusudiwa.

Kwa upande wake Rais wa Tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso amesema fungu ambalo limeongezwa kwenye mfuko wa madeni litasaidia kuweka ulinzi kwenye kuimarisha uchumi wa Ulaya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani IMF Christine Lagarde ni miongoni mwa wale ambao walihudhuria mkutano huo huko Brussels ambaye naye alipongeza hatua ambayo imefikiwa akiamini itasaidia kuokoa uchumi wa Ulaya na dunia kwa ujumla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.