Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Virusi vya Corona: Idadi yawaliofariki dunia yaongezeka, hofu yazidi kutanda duniani

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa ugonjwa hatari unaofahamika kama 'Corona' imeongezeka hadi 106 na karibu kesi 1,300 mpya za maambukizi zimeripotiwa, kwa mujibu wa serikali ya China.

China imeweka marufuku ya kusafiri ili kuzuia maambukizi zaidi.
China imeweka marufuku ya kusafiri ili kuzuia maambukizi zaidi. NICOLAS ASFOURI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mtu wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa huo amefariki dunia katika mji wa Beijing, nchini China huku mwengine mmoja nchini Ujerumani. Wasiwasi umetanda ulimwenguni kote kutokana na ugonjwa huo, na hatua za tahadhari zimeendelea kuchukuliwa kwenye mipaka, wakati shirika la Afya Duniani (WHO) likichukulia ugonjwa huo kama 'kitisho kikubwa kwa ulimwengu'.

Wasiwasi umetanda ulimwenguni kote na nchi nyingi zichukua hatua za tahadhari kwenye mipaka au kushauri raia wao kutosafiri kwenda nchini China, ya mtu wa kwanza aliyeambuykizwa virusi vya ugonjwa huo kufariki dunia huko Beijing.

Kufikia Jumatatu hii Januari 27, idadi ya vifo ilikuwa 106 na karibu kesi mpya 1,300 zimethibitishwa. Kwa sasa watu 4,000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa hatari unaofahamika kaka 'Corona' nchini China. Karibu wagonjwa wengine hamsini wameripotiwa katika baadhi ya nchi dunia, ambapo baadhi ya watu kutoka mataifa kadhaa wameambukizwa virusi, hususan katika bara la Asia, Australia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

Mlipuko wa ugonjwa huu umekuja wakati wa sherehe za mwaka mpya ambazo huwakutanisha mamilioni ya watu nchini humo wakisafiri kuwatembelea ndugu na marafiki.

Sherehe za mwaka mpya zilisogezwa mbele kwa siku tatu mpaka siku ya Jumapili, ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.