Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-MAJANGA YA ASILI

Australia kukabiliwa na wimbi jipya la joto kali

Wimbi jipya la joto linatarajiwa kupiga Ijumaa nchini Australia na kuzidisha hali mbaya kwa sababu yaathiri kwa miezi kadhaa Kusini na Mashariki mwa nchi.

Australia yaendelea kukumbwa na visa vya moto.
Australia yaendelea kukumbwa na visa vya moto. SAEED KHAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Joto kali na ukame vimesababisha moto wa nyika nchini Australia kwa kipindi cha miezi kadhaa, lakini hali ya ukame ya nchi hiyo imekuwepo kwa miaka kadhaa.

Mamlaka imewasihi wananchi kuwa waangalifu.

Majimbo ya Victoria na New South Wales yatashuhudia kiwango cha joto kikifikia 40 ° C.

Upepo pia unatarajiwa kupiga kusini ili kuzidisha hali hiyo.

"Mazingira yatakuwa magumu. Upepo mkali na utasababisha hali kuwa mbaya zaidi," mkuu wa idara ya Zima Moto katika JImbo la New South Wales, Shane Fitzsimmons, amewaambia waandishi wa habari.

Imeelezwa kuwa kutokana na hali ya ukame ngamia wamekuwa tishio kwenye jamii hivyo unahitajika udhibiti wa haraka.

Jamii zinazoishi karibu na makazi ya ngamia hao wamesema wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu, kwa sababu ngamia hubomoa uzio, huzunguka nyumba wakijaribu kupata maji kupitia maji yanayodondoka kutoka kwenye viyoyozi.

Karibu makazi 2,000 yameharibiwa kutokana na moto uliodumu kwa miezi kadhaa.

Karibu watu 25 wameuawa tangu mwezi Septemba.

Maeneo ya mashariki na kusini mwa Australia yameharibiwa vibaya- na wanyama wengi wameuawa kwa moto.

Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na joto kali katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni na hali inatarajiwa kuendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.