Pata taarifa kuu
LEBANON-JAPAN-GHOSN-HAKI

Carlos Ghosn awasili Beirut licha ya kupewa masharti ya kutoka nje ya Japan

Mwenyekiti wa zamani wa makampuni ya magari ya Renault-Nissan kwa sasa yuko nchini Lebanon, amewasili Beirut kwa ndege ya kibinafsi. Mfanyabiashara huyo wa zamani anayeshutumiwa kwa ufisadi na mahakama ya Japani na kupewa kifungo cha nyumbani jijini Tokyo, aliondoka Japani katika mazingira yasiyoeleweka.

Carlos Ghosn Machi 6, 2019 huko Tokyo, baada ya kuachiliwa kwa dhamana.
Carlos Ghosn Machi 6, 2019 huko Tokyo, baada ya kuachiliwa kwa dhamana. REUTERS/Issei Kato/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Sikukimbia mahakama - nimekimbia dhulma na mateso ya kisiasa, " amesema Carlos Ghosn.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari, mwenyekiti wa zamani wa makampuni ya magari Renault-Nissan amethibitisha kwamba yuko nchini Lebanon.

Carlos Ghosn amesema kuwa hataki tena "kushikwa mateka na mfumo wa mahakama ya Japan" na anapanga kukutana na vyombo vya habari wiki ijayo.

Saa chache kabla ya taarifa ya Carlos Ghosn, gazeti la Financial Times, likimnukuu mshirika wa mwenyekiti wa zamani wa Renault-Nissan, limeripoti kwamba mfanyabiashara huyo wa zamani aliwasili Beirut Jumapili Desemba 29 jioni na ndege ya kibinafsi akitokea Uturuki.

Taarifa ambayo imethibitishwa muda mfupi baadaye na chanzo cha usalama cha Lebanon, kikilithibitishia shirika la habari la AFP kwamba Carlos Ghosn "aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Beirut siku ya Jumapili". Na afisa mwingine wa Lebanon ameongeza kwamba "mfumo uliotumiwa Carlos Ghosn kutoka Japan haueleweki".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.