Pata taarifa kuu
UFILIPINO-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Phanfone chaua watu wasiopungua 16 Ufilipino

Kimbunga Phanfone, ambacho kimepiga katika vijiji vya watu wenye maisha duni na maeneo ya kitalii katikati mwa Ufilipino siku ya Krismasi, kimeua watu wasiopungua 16, viongozi wa eneo hilo wamesema leo Alhamisi.

Nyumba iliyoharibiwa na kimbunga Phanfone huko Ormoc City (Ufilipino) Desemba 25, 2019.
Nyumba iliyoharibiwa na kimbunga Phanfone huko Ormoc City (Ufilipino) Desemba 25, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kimbunga hiki, ambacho kiliambatana na upepo mkali ambao ulikua unavuma kwa kasi hadi kilomita 195 kwa saa, kimesababisha uharibifu mkubwa, na huku kiking'oa paa za nyumba na kuharibu baadhi ya mitambo ya umeme.

Katika maeneo yaliyoathirika zaidi, mitandao ya intaneti na simu bado imekataa.

Watu wasiopungua 16 wanaoishi katika vijiji au miji katika visiwa vya Visayas katikati mwa nchi wameuawa, maafisa wa mamlaka inayosiamia majanga wamesema.

Kimbunga Phanfone kimepiga kisiwa kidogo cha Boracay, katikati mwa nchi, (kisiwa cha Coron, magharibi) na maeneo mengine maarufu sana kwa watalii, haswa wageni, kwa fukwe za mchanga mweupe.

Uwanja wa ndege wa Kalibo, umeathirika zaidi, kwa mujibu wa mtalii kutka Korea ambaye alijikuta amekwama na kutoa picha kwa shirika la habari la AFP.

'Barabara hazipiti lakini shughuli ya kusafisha barabara inatarajia kuanza. hali ni mbaya kabisa,' amesema Jung Byung Joon kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

'Kila kitu kilicho ndani ya eneo la chini ya mita 100 linalozunguka uwanja wa ndege kimeharibiwa. Kwenye uwanja wa ndege, watu wengi wamekata tamaa kwa sababu safari zao zimefutwa,' Jung Byung Joon amesema.

Mwaka 2013 kimbunga Haiyan kiliua watu zaidi ya 7,300 nchini Ufilipino hasawa katika mji wa Tacloban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.