Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI- JAPAN-USHIRIKIANO

Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora lake

Saa chache baada ya kutangazwa kuanza tena kwa mazungumzo ya nyuklia na Marekani, Korea Kaskazini imefanya jaribio jipya la kurusha hewani kombora la masafa marefu mapema Jumatano hii asubuhi. Kombora hilo limesafiri hewani hadi eneo la kiuchumi la Japan.

Raia wa Korea Kusini wakitazama kwnye televisheni tangazo la Korea Kaskazini la kurusha kombora toka ardhini kwenda hewani, Seoul, Oktoba 2, 2019.
Raia wa Korea Kusini wakitazama kwnye televisheni tangazo la Korea Kaskazini la kurusha kombora toka ardhini kwenda hewani, Seoul, Oktoba 2, 2019. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Ni miaka miwili sasa tangu serikali ya Korea Kaskazini isitishe kufanya majaribio ya makombora yake kwa kuyarusha kutoka ardhini kwenda hewani.

Ofisi ya rais nchini Korea Kusini imesema leo asubuhi kwamba Korea Kaskazini imerusha kombora lililotarajiwa kurushwa na chombo cha majini kutoka baharini. Kombora hilo limerushwa kutoka mji wa bandari wa Wonsan, hadi kwenye Bahari ya Japan.

Kombora hilo, linaloshukiwa kuwa ni la aina mpya, limekwenda juu sana hewani, hadi kilomita 910. na limesafiri kilomita 450 kabla ya kudondoka katika eneo la kipekee la uchumi la Japan. Hii ni mara ya kwanza katika miaka miwili kombora la Korea Kaskazini linakwenda mbali kiasi hicho.

Waziri Nkuu wa Japan Shinzo Abe amelani kitendo hico cha Korea Kaskazini na kutaja kitendo hicho kama "ukiukwaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa".

Uchokozi huo unaelezwa kama njia ya serikali ya Korea Kaskazini kuonyesha uwezo wake wa kijeshi na kuweka shinikizo kwa Marekani, kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya nyuklia yaliyopangwa kufanyika Jumamosi, na ambayo yalizubiriwa kwa miezi kadhaa.

Korea Kaskazini inataka kukaa kwenye meza ya mazungumzo baada ya kuonyesha nguvu zake za kijeshi, ameongeza Shinzo Abe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.