rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Maandamano nchini Iraq: Takwimu rasmi za watu waliouawa ni 157, pamoja na 111 Baghdad
  • Machafuko Chile: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 15 baada ya watu watatu kuuawa (serikali)

HONG KONG

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi yashtumiwa kutumia risasi za moto kwa kuwatawanya waandamanaji Hong Kong

media
Oktoba 1 imetajwa na waandamanaji Hong Kong, kuwa ni siku ya hasirawakati Beijing ikiadhimisha miaka 70 tangu China kuasisiwa. REUTERS/Jorge Silva

Waandamanaji katika eneo la Hong Kong, wamekuwa wakikabiliana na polisi huku ripoti zikisema kuwa mmoja kati ya waandamanaji amepigwa risasi kifuani na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya.


Makabiliano haya yamekuja, wakati China inapoadhimisha miaka 70 ya chama cha Kikomunisti nchini humo.

Awali, polisi wamekuwa wakitumia risasi za mpira kukabiliana na waandamanaji na hii ndio mara ya kwanza kwa risasi za moto kutumiwa kutuliza maandamano hayo.

Maandamano ya leo yametatiza shughuli za kawaida katika jiji hilo, huku barabara zikifungwa, uahribu mkubwa ukiripotiwa hasa kuharibika kwa majengo.

Kwa muda wa miezi minne maandamano yamekuwa yakiendelea, huku rais wa China Xi Jinping akisema kuwa hakuna anayewezesha kuligawa taifa hilo.

Kila tarehe moja mwezi Oktoba, kumeendelea kushuhudiwa kwa maandamano makubwa dhidi ya serikali ya China, katika eneo hilo ambalo Beijing imekuwa ikiongoza tangu mwaka 1997.

Licha ya Hong Kong kuwa sehemu ya China, waandamanaji mara kwa mara wameendelea kupinga kutawaliwa na China kwa kile wanachokisema kuwa, wanataka kujiongoza na kuendeleza demokrasia.