rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Iran Marekani Hassan Rouhani Donald Trump Emmanuel Macron

Imechapishwa • Imehaririwa

Iran kujadiliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

media
Marais wa Ufaransa na Irani, Emmanuel Macron na Hassan Rohani, Septemba 23, 2019 New York kando na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. LUDOVIC MARIN / AFP

Mkutano Mkuu wa 74 wa kila Mwaka wa Umoja wa Mataifa unafunguliwa leo Jumanne, Septemba 24 mjini New York. Viongozi mbalimbali wanatarajia kupishana kwa kuhutubia ulimwengu hadi Jumatatu wiki ijayo.


Hotuba za Marais Donald Trump na Emmanuel Macron zinasubiriwa kwa hamu na gamu, hususan kuhusu suala la Iran, ambalo limejadiliwa sana katika saa zahivi karibuni. Shiniko ni kubwa dhidi ya Tehran.

Kando ya Mkutano Mkuu wa Umpoja wa Mataifa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaendelea na juhudi zake za kujaribu kupunguza mvutano kati ya Washington na Tehran, ambayo inashutumiwa kuwa hakuheshimu tena mkataba wa nyuklia, kwa kulipiza kisasi kwa vikwazo vya Marekani dhidi yake.

Jumatatu, Septemba 23, Rais wa Ufaransa alikutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Iran, Hassan Rohani, katika hoteli iliyo karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Mazungumzo yao yalidumu saa mbili.

Mbele ya waandishi wa habari, viongozi hao wawili walipena mikono kwa furaha.

Lakini, saa machache kabla, Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kwa kuunga mkono Washington, waliinua sauti zao dhidi ya seriklai ya Tehran.

Viongozi hao walitoa taarifa ya pamoja ikionyesha wazi kuwa Iran ndiyo iliyohusika na mashambulio dhid ya mitambo ya mafuta ya Saudi Arabia, na kuitaka Tehran kujizuia na "uchochezi wowote " dhidi ya hasimu wake mkubwa katika ukand wa Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzanke wa Marekani Donald Trump wanatarajia kukutana leo Jumanne.

Rais wa Ufaransa, pia alimwambia Rais Rohani kwamba njia ya kuondokana na mvutano ipo. "Wakati umefika kwa Iran kutumia nafasi hiyo, amebaini Emmanuel Macron. Lakini washirika wa karibu wa rais wa Ufaransa, hawana imani kabisa na uwezekano wa kufanyika kwa mkutano mjini New York kati ya Rais Donald Trump na Hassan Rohani, unaopendekezwa na Paris.

Rais wa Marekani alimjibu Emmanuel Macron, akisema hahitaji mpatanishi na kwamba kwa sasa, hakuna mkutano wowote uliopo kwenye ajenda, hata ikiwa mlango haujafungwa kabisa.

Rais Macron ataendeleza juhudi zake za upatanishi hadi kuondoka kwake nchini Marekani Jumanne hii usiku.