rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Iran Marekani Hassan Rouhani Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Rohani atoa wito kwa Marekani "kuchukuwa hatua ya kwanza" kuondoa vikwazo

media
Picha iliyotolewa na ofisi ya rais wa Irani Agosti 27, 2019 ikimuonyesha Rais Hassan Rohani (wa pili kutoka kushoto) akihudhuria sherehe katika mji mkuu Tehran. © AFP

Rais wa Irani Hassan Rohani ameitaka Marekani "kuchukuwa hatua ya kwanza kuondoa vikwazo vyote" dhidi ya nchi yake, siku moja baada ya tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuwa yuko tayari kushiriki mkutano na kiongozi huyo wa Irani.


Hatua ya kwanza ni kuondoa vikwazo. Unapaswa kuondoa vikwazo vyote visivyo halali, visivyo kuwa na haki na ambavyo vimepitwa na wakati dhidi ya taifa la Irani, "Rohani amesema katika hotuba iliyorushwa kwenye runinga ya serikali.

Vikwanzo hivyo viliwekwa na Washington baada ya uamuzi wake wa kujiondoa kwa hiari yake kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran mnamo mwaka 2018, mkataba uliyofikiwa mnamo mwaka 2015 katika mji wa Vienna.

Kwa miezi kadhaa, mvutano umeendelea kuongezeka kati ya Tehran na Washington.

Jumatatu wiki hii, kwa kuhitimisha mkutano wa kilele wa mataifa yaliostawi zaidi kiuchumi duniani (G7), nchini Ufaransa, rais wa Marekani, hata hivyo, alisikika akisema kuwa kutokana na mzozo wa Iran, anaona kuwa yuko tayari kushiriki mkutano ujao na Bw Rohani.