rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

HONG KONG

Imechapishwa • Imehaririwa

Kiongozi wa Hong Kong aonya waandamanaji

media
Waandamanaji wakiendelea na maandamano HOng Kong Agosti 5, 2019. REUTERS/Kim Kyung-Hoon

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam ameonya kuwa maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea kwenye mji huo, yanaharibu uchumi.


Bi.Lam ametoa kauli hii wakati huu mgomo wa siku tatu ukianza katika uwanja wa ndege wa Hong Kong.

Aidha, kiongozi huyo wa Hong Kong ameapa kuwa licha ya maandamano hayo kuendelea, uongozi wake haupo tayari kulegeza kamba kuhusu matakwa ya waandamanaji.

Waandamanaji wamekuwa na mkutano na wafanyibiashara katika mji huo na kuhamasisha wakaazi wa Hong Kong kwenda katika uwanja wa ndege kukaa kwa siku tatu, ili kupata uungwaji mkono wa kimataifa.

Wanaharakati huko Hing Kong, wanapinga mpango wa uongozi wa eneo hilo kupitisha sheria ambayo itaruhusu wakaazi wa eno hilo kushtakiwa nchini China, kwa kile wanachosema, wanaolengwa ni wapinzani wa serikali ya Beijing.

Serikali ya China inasema haitavumlia kuendelea kushuhudiwa kwa maandamano hayo wanayosema yanaharibu mji huo.