Pata taarifa kuu
PAKISTANI-INDIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Pakistan yaashutumu India kwa kutumia itikadi kali za kibaguzi

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameapa kupinga uamuzi wa serikali ya India kuondoa uhalali wa jimbo linalojitegemea la Kashmiri, vita ambavyo amesema atavipeleka katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wafuasi wa chama cha siasa cha kidini Jamaat-e-Islami (JI) wakiimba nyimbo zinazopinga serikali ya India wakati wa maandamano Islamabad Agosti 6, 2019, siku moja baada ya India kutupilia mbali hoja ya kujitawala kwa Jimbo la  Kashmir.
Wafuasi wa chama cha siasa cha kidini Jamaat-e-Islami (JI) wakiimba nyimbo zinazopinga serikali ya India wakati wa maandamano Islamabad Agosti 6, 2019, siku moja baada ya India kutupilia mbali hoja ya kujitawala kwa Jimbo la Kashmir. AAMIR QURESHI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Khan amesema hatua hiyo ya India haikubaliki na inakwenda kinyume cha sheria za kibinadamu, na kuelekeza kuwa kinachoendelea ni mauaji ya kikabila.

Shughuli zimekwama katika jimbo hilo, baada ya uamuzi huo tata wa India.

Kashmir ni jimbo ambalo linawaniwa na nchi ya India na Pakistan, na ni eneo la mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Hali hii imeendelea kusababisha utovu wa usalama katika jimbo hilo kwa kuwepo kwa kundi la wapiganaji ambalo kwa zaidi ya miaka 30, limewauwa maelfu ya watu.

Mbali na Pakistan, nchi jirani ya China pia imelaani hatua hiyo na kusema haikubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.