rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Iran EU Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Iran: Mkutano wa dharura wa Vienna ulikuwa muhumu

media
Mkutano wa dharura Jumapili, Julai 28 Vienna, mkutano uliojumuisha nchi zilizotia saini kwenye mpango wa pamoja kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran. REUTERS/Kirsti Knolle

Mkutano wa dharura Jumapili uliojumuisha nchi zilizotia saini kwenye mpango wa pamoja wa mkataba wa nyuklia wa Iran uliofanyika mjini Vienna, umekuwa "mzuri" kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi.


Hata hivyo Teheran imesema itaendelea kupunguza ahadi zake katika sekta hiyo ikiwa nchi za Ulaya zitashindwa kuokoa mkataba huo ambao Marekani ilijiondoa.

Katika wiki za hivi karibuni, Nchi za Ulaya zilielezea utayari wao wa kufanya kila waliwezalo ili kuokoa mkataba huo, lakini hawakuficha wasiwasi wao kuhusu uamuzi wa Iran wa hivi karibuni wa kuvunja ahadi zake, hasa kwa kurutubisha uranium yenye utajiri kwa 4.5%, kiwango kilichopigwa marufuku na mkataba huo.

Iran, inayoendelea kuathiriwa na vikwazo vya Marekani, imeomba nchi za Ulaya kuisaidia vikwazo hivyo visitishwe, kwa kuiruhusu kuuza hasa mafuta yake nje ya nchi.

Katika suala hili, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameonya nchi za Ulaya baada ya mkutano huo akisema: "Kizuizi chochote kwa njia ambayo Iran inauza mafuta yake kinakwenda kinyume na" mkataba wa nyuklia, ameelezea Abbas Araghchi, akimaanisha kukamatwa mapema mwezi Julai meli ya mafuta ya Iran na mamlaka ya Uingereza kwenye pwani ya Gibraltar.

Licha ya malalamiko kutoka pande zote, mazungumzo yalikuwa "mazuri". Mkutano mpya wa tume ya pamoja unaweza kuitishwa, katika ngazi ya mawaziri, katika wiki zijazo.