Pata taarifa kuu
UFILIPINO-AMNESTY-HAKI

Amnesty yalaani vita vya Duterte dhidi ya madawa ya kulevya

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International limelaani vita vinavyoendeshwa na rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, dhidi ya madawa ya kulevya.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, Agosti 8, 2018 Manila wakati wa maadhimisho ya miaka 117 ya kuanzishwa kwa polisi ya Ufilipino.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, Agosti 8, 2018 Manila wakati wa maadhimisho ya miaka 117 ya kuanzishwa kwa polisi ya Ufilipino. TED ALJIBE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International inasema watu elfu sita mia sita wameuawa katika vita hivyo vya rais Duterte. Kwa mujibu wa mashirika yanayotetea haki za binadamu, idadi hiyo ni ndogo kulingana na taarifa walizokusanya. Rais Rodrigo Duterte, ambaye alizindua operesheni hiyo mbaya mnamo mwaka 2016, hataki kuachia.

Hivi karibuni aliahidi kuwa "miaka mitatu ijayo ya muhula wake itakuwa hatari zaidi kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na wafanyabiashara".

Katika ripoti iliyochapishwa Jumatatu hii, Julai 8, Amnesty International inalaani jinsi "vita" hivyo vinavyoendeshwa, na inaweka mbele mkakati mzuri unaoeleweka.

Mkakati huo unatakiwa kuanza kuhudumia wananchi wa Ufilipino walio masikini zaidi, amesema Rachel Chhoa-Howard, ambaye ni mongoni mwa walioandika ripoti ya Amnesty: "Wanalengwa tu kwa sababu hawawezi kujitetea wenyewe. Ni watu ambao ni rahisi kulengwa. Polisi mara kwa mara huchapisha takwimu kuhusu idadi ya watu waliouawa katika operesheni hiyo. Hii ni kuonyesha kwamba "vita dhidi ya madawa ya kulevya" imefanikiwa.

Wanaharakati wa haki za bindamu wanasema ahadi ya Duterte ya kuwauwa maelfu ya wale wanaojishughulisha na madawa ya kulevya imepelekea polisi kufanya mauaji yaliyovuka mpaka dhidi ya wanaoshukiwa kuwa ni watumiaji na wafanya biashara wa madawa hayo.

Hata hivyo polisi wamekanusha tuhuma hizo za mauaji na wanasisitiza kuwa wamekuwa wakiwauwa washukiwa ambao walikuwa na silaha kwa kujihami wao wenyewe katika operesheni halali ya kupambana na madawa ya kulevya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.