rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Iran Marekani Hassan Rouhani Donald Trump Ayatollah Ali Khamenei

Imechapishwa • Imehaririwa

Iran yalaani vikwazo vya Marekani

media
Rais wa Iran Hassan Rouhani,amjia juu rais wa Marekani Donald Trump kufuatia vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya nchi yake.. Official President website/Handout via REUTERS

Iran imelaani hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya na kusema hatua kama hiyo isiyo ya maana na inaonesha kuwa Marekani imekuwa ikidangaya kuwa iko tayari kufanya mazungumzo.


Rais wa Iran amesema kuwa hatua ya Marekani inaonesha kuwa, rais Donald Trump hafikirii vizuri na mgumu wa kuelewa.

Siku ya Jumatatu, Trump alimwekea vikwazo kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na wakuu wa jeshi nchini humo na kuonya kuwa itatangaza vikwazo dhidi ya Waziri wa Mambo ya nje Mohammad Javad.

Urusi imelaani hatua hiyo ya Marekani na kusema inasimama na Iran, huku Ufaransa ikionya Iran dhidi ya kuendelea na mpango wa kurutubisha uranium kinyume na mkataba wa mwaka 2015.

Wasi wasi kati ya Marekani na Iran umekuwa ukishuhudiwa tangu mwaka uliopita baada ya rais Trump kujiondoa kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu nyuklia, na kurejesha vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Iran.

Hali ilionekana kuwa mbaya wiki iliyopita, baada ya ndege ya kivita ya Marekani isiyo kuwa na rubani kuangushwa na Iran.

Kumekuwa na wasiwasi wa mataifa haya mawili kuingia kwenye vita lakini Marekani imekuwa ikisema haitaki vita.