rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Iran Mike Pompeo Mohammad Javad Zarif

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran

media
Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema ramani iliyochapishwa na Bw Zarif ni ya "kitoto". REUTERS/Leah Millis

Marekani inatarajia kutangaza leo Jumatatu vikwazo "vikuu" vipya dhidi ya Iran, wakati mvutano unaendelea kuongezeka kati ya nchi hizi mbili, na hivyo kusababisha hofu ya kuzuka vita kati ya mahasimu hao wawili.


Hata hivyo Tehran na Washington wameendelea kusema kuwa hawana nia ya kuanzisha vita, wakati kumeendelea kushuhudiwa matukio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya meli ya mafuta ambayo chanzo chake hakikujulikana na hatua ya Iran kuangusha ndege isiyo kuwa na rubani ya Marekani katika eneo Ghuba.

Jumapili, waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alibaini kwamba kwa mara ya kwanza tukio lililohusisha ndege isiyo kuwa na rubani ya Marekani Mei 26, ambayo kulingana na ramani aliyoshapisha kwenye akaunti yake ya Twitter, ilifanya dakika takribani 20 ikiwa juu ya anga la Iran na kwamba ilitahadhariswa mara tatu.

Kabla ya kusafiri kwenda Saudi Arabia na Falme za Kiarabu, Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema ramani iliyochapishwa na Bw Zarif ni ya "kitoto".

Tangazo la Iran linakuja baada ya kuangusha ndege isiyo kuwa na rubani ya Marekani siku ya Alhamisi. Tehran inadai kwamba ndege hiyo ilikiuka sheria kwa kuingia katika anga yake.