rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

HONG KONG China Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Maelfu ya waandamanaji jijini Hong Kong wazingira makao makuu ya jeshi la Polisi

media
Waandamanaji wa Hong Kong 路透社

Maelfu ya waandamanaji wamezingira makao makuu ya polisi jijini Hong Kong wakiendelea kushinikiza kutupiliwa mbali kwa mswada tata unaoruhusu washtakiwa wa makosa mbalimbali kufikishwa mashtaka nchini China.


Polisi wametoa wito kwa waandamanaji, kuondoka kwa amani, kwa kile wanachosema kuwa, uwepo wao utatatiza shughuli za dharura.

Mamilioni ya waandamanaji wameendelea kuandamana katika siku za hivi karibuni, wakiendelea kuushinikiza uongozi wa Hong Kong kuachana kabisa na mswada huo.

Carrie Lam kiongozi wa Hong Kong na mwakilishi wa China, katika eneo hilo amesitisha mswada huo kuendelea kujadiliwa na wabunge na kupitishwa lakini hajasema iwapo umesitishwa.

Wanaharakati wakiongozwa na Joshua Wong ambaye ni mwanafunzi, wameendelea kusisitiza kuendelea kuandamana hadi pale mswada huo utakapotuliwa mbali, lakini pia wanamtaka Bi. Lam kujiuzulu.

Wapinzani wa serikali ya China wanaoishi Hong Kong, ambayo ilikabidhiwa kwa China mwaka 1997, wanadai kuwa mswada huo unawalenga.