rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

China Korea Kaskazini Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa China Xi Jinping azuru Korea Kaskazini

media
Raos wa China China Xi Jinping akisalimiana na mwenyeji wake Kim Jong Un jijini Pyonyang Juni 20 2019 AFP

Rais wa China Xi Jinping anazuru Korea Kaskazini kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.


Viongozi hawa wawili wanakutana katika kikao chao cha tano kwa kipindi cha miezi 10 sasa.

Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza kwa rais wa China kutembelea Korea Kaskazini ndani ya miaka 14.

Xi Jinping atakuwa kwa ziara ya siku mbili jijini Pyongyang, ambapo watajadiliana kuhusu mradi wa Nyuklia, masuala ya amani na ushirikiano wa kibiashara na uchumi.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanasema kuwa ziara hii ni kutuma ujumbe wa kidiplomasia kwa nchi ya Marekani.

Mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini, hayajaonekana kupata mwafaka licha ya Kim Jong Un na Donald Trump kukutana mara mbili bila mafanikio.

Marekani imeendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Korea Kaskazini licha ya nchi hiyo kusitisha majaribio yake ya silaha za nyuklia.