rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Malaysia Ukraine Uholanzi

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu wanne kushtakiwa kwa kuiangusha ndege ya Malaysia mwaka 2014

media
Baada ya ndege ya abiria kuanguashwa nchini Ukraine PHOTO | COURTESY

Washukiwa wanne, wanaominiwa kuhusika na kuiangusha ndege ya abiria ya Malaysia MH17 mwaka 2014  nchini Ukraine, wametajwa na watafunguliwa mashtaka.


Raia watatu wa Urusi, na mmoja wa Ukraine, watafunguliwa  mashataka ya kusafirisha kombora lililosababisha kuiangusha ndege hiyo na kusababisha vifo vya watu 298.

Ndege hiyo ya abiria ilikuwa imetokea mjini Amsterdam nchini Uholanzi kwenda nchini Kuala Lumpur, wakati ilipoangushwa katika angaa la Mashariki mwa Ukraine wakati wa mzozo kati ya nchi hiyo na Urusi.

Wanne hao ambao wametajwa kuwa Igor Girkin, Sergey Dubinskiy na Oleg Pulatov wote raia wa Urusi na Leonid Kharchenko kutoka Ukraine, watafikishwa Mahakamani nchini Uholanzi kuanzia tarehe 9 mwezi Machi mwaka 2020.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa washukiwa hao imetangazwa.