rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

HONG KONG China Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Waandamanaji Hong Kong, waapa kuendelea kuandamana

media
Waandamanaji, Hong Kong katika siku zilizopita 路透社。

Maelfu ya waandamanaji katika eneo linalojitawala la Hong Kong, wameapa kuendelea na maandamano siku ya Jumapili licha ya serikali ya eneo hilo kuamua kusitisha mswada tata kuhusu kusafirishwa kwa washukiwa wa makosa mbalimbali kwenda katika Mahakama za China.


Aidha, waandamanaji hao wanamtaka kiongozi wa Hong Kong Bi. Carrie Lam ajiuzulu na kuachana kabisa na mswada huo ambao umezua maandamano makubwa ya kuupinga kwa siku kadhaa sasa.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa Hong Kong, hakusema iwapo mswada huo hautarejelewa tena hali inayozua wasiwasi kuwa huenda ukarudishwa tena katika siku zijazo.

Mswada huo umezua maandamano makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa muda mrefu huko Hong Kong eneo ambalo waakazi wameonekana kupingana na sera za China hasa kuhusu demokrasia na uongozi.

Hong Kong ni Koloni ya Uingereza, lakini mwaka 1997 ilirejeshwa chini ya utawala wa China, chini ya sera ya nchi moja ya China.

Wanaharakati wa upinzani wamekuwa wakisema kuwa, mswada huo unawalenga kwa sababu ya upinzani wao kuhusu uongozi wa Beijing.