Pata taarifa kuu
HONG KONG

China: Waandamanaji wazuia bunge kujadili sheria tata

Maelfu ya waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wamezuia njia zinazoingia katika ofisi za makao makuu ya Serikali na Bunge na kulazimisha mamlaka kuahirisha mjadala kuhusu sheria tata ya kubadilishana na wahalifu.

Waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wakiwa nje ya makao makuu ya ofisi za Serikali na Bunge wakipinga sheria tata ya kubadilishana wahalifu. Juni 12, 2019.
Waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wakiwa nje ya makao makuu ya ofisi za Serikali na Bunge wakipinga sheria tata ya kubadilishana wahalifu. Juni 12, 2019. REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Wakiwa wamevalia mavazi meusi na kofia nguvu za kichwa, waandamanaji walikabiliana na polisi waliokuwa nje ya ukumbi wa bunge kujaribu kuwazuia maelfu ya raia wasiingie katika njia za makao makuu ya Serikali.

Mpaka kufikia majira ya asubuhi ya Jumatano, njia zote za kuelekea kwenye ukumbi wa bunge na ofisi za Serikali zilikuwa zimezingirwa na kujaa waandamanaji waliokuwa na mabango wakidai uhuru.

Maandamano ya hivi leo yamechelewesha mjadala wa bungeni ambapo wabuneg walitakiwa kujadili sheria ya kubadilishana wahalifu na Serikali ya Beijing, ambapo unatakiwa kupigiwa kura Juni 20.

Wakiwa wamejihami kwa mabango na vizuizi, waandamanaji walikuwa waakimba nyimbo za kimapunduzi na kuukashifu utawala wa Beijing kwa kujaribu kuingilia masuala yake ya ndani.

Mpaka sasa hakuna taarifa za polisi kutumia mabomu ya kutoa machofu au maji ya pilipili kujaribu kukabiliana na waandanaji ambao wameapa kuhakikisha sheria hiyo haipitishwi.

Sheria hii ambayo itashuhudia ubadilishanaji wa wahalifu kati ya bara na Hong Kong, imeoenakana kuwagawa hata wanasheria ambao baadhi wanaiunga mkono huku wengine wakiipinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.