rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sri Lanka

Imechapishwa • Imehaririwa

Ulinzi waendelea kuimarishwa Sri Lanka

media
waombolezaji walifanya ibada kuwakumbuka ndugu na marafiki zao waliopoteza maisha katika shambulio la juma lililopita ambapo watu 253 waliuawa. REUTERS/Thomas Peter

Waumini wa madhehebu ya Kikristo nchini Sri Lanka, siku ya Jumapili wamelazimika kufanya misa wakiwa majumbani mwao baada ya Serikali kuzuia kufunguliwa kwa makanisa.


Uamuzi wa Serikali umetokana na hofu ya kutekelezwa kwa mashambulizi zaidi, huku viongozi wa makanisa wakikashifu shambulio la juma lililopita, wakisema lilikuwa ni udhalilishaji na halina utu.

Serikali ya Sri Lanka imetetea uamuzi wake ikisema imelazimika kuchukua tahadhari kutokana na kuwepo kwa wasiwasi wa kutekelezwa kwa mashambulizi mengine ya kigaidi kulenga makanisa.

Ulinzi uliimarishwa kwenye makanisa mengi ambapo waombolezaji walifanya ibada kuwakumbuka ndugu na marafiki zao waliopoteza maisha katika shambulio la juma lililopita ambapo watu 253 waliuawa.