rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sri Lanka Maithripata Sirisena

Imechapishwa • Imehaririwa

Mashambulizi Sri Lanka: Serikali yakiri makosa

media
Wapolisi wa Sri Lanka wanakaguwa katika nyumba ya familia ya mmoja wa watuhumiwa wa mashambulizi ya Jumapili, Colombo Aprili 25, 2019. REUTERS/Thomas Peter

Nchini Sri Lanka, uchunguzi unaendelea kujaribu kutambua watu waliohusika katika mashambulizi ya Jumapili iliyopita ambayo yaligharimu maisha ya watu 359. Polisi imeendelea kuwakamata washukiwa wa mauaji hayo.


Serikali ya Sri Lanka imekiri kuwa, kulikuwa na kuupuzwa kwa taarifa za kiiteljensia kabla ya shambulizi la bomu wakati wa sikukuu ya Pasaka, lililosababisha vifo vya watu 359 na kusababisha watu wengine 500 kujeruhiwa.

Ripoti zinasema kuwa, Inteljensia kutoka nchini India, zilieleza kuwa kulikuwa na uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya bomu yakilenga makanisa na hoteli, na taarifa hiyo iliwafikia wakuu wa usalama nchini humo.

Rais Maithripata Sirisena amemfuta kazi Waziri wa Ulinzi na Inspekta Mkuu wa Polisi kutokana na shambulizi hilo baya.

Washambuliaji nane kati ya tisa wanaoaminiwa walihusika, wote ni rais wa Sri Lanka.

Kwa sasa uhusiano si mzuri kati ya jamii ya Wakristo na Waislamu, hku serikali ikijaribu kuimarisha msikamano kati ya jamii hizo mbili.