Pata taarifa kuu
SRI LANKA-UGAIDI

Sri Lanka: Watu zaidi ya 136 wauawa katika mashambulizi yaliyolenga makanisa na hoteli

Mfululizo wa milipuko iliyolenga makanisa na hotel wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka nchini Sri Lanka, imesababisha vifo vya watu zaidi ya 156 huku wengine zaidi ya 400 wakijeruhiwa.

Mwanajeshi wa Sri Lanka akilinda eneo la kanisa lililoshambuliwa, 21 Aprili 2019
Mwanajeshi wa Sri Lanka akilinda eneo la kanisa lililoshambuliwa, 21 Aprili 2019 REUTERS/Dinuka Liyanawatte
Matangazo ya kibiashara

Polisi inasema miongoni mwa waliopoteza maisha, wamo raia wa kigeni 35.

Waziri mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe amelaanimashambulizi haya yaliyoonekana kupangwa, akiyaita ni mashambulizi ya kibaguzi yaliyolenga kuwajengea hofu raia.

Picha za mnato na zile za video ambazo zimeendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha uharibifu mkubwa uliosababishwa na milipuko hiyo hasa kwenye makanisa ambako waumini wa Kikristo walikuwa kwenye ibada ya Pasaka.

Mapaa ya makanisa karibu matatu yaliyolengwa yameonekana kuharibiwa vibaya kutokana na nguvu ya milipuko yenyewe, huku miili na damu zikiwa zimetapakaa kila mahali kwenye eneo la tukio.

Watu waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospital ya kitaifa ya mjini Colombo kutokana na hospitali nyingi za kwenye miji ambayo mashambulizi haya yametekelezwa hazina uwezo wa kuhudumia watu wote na wale wanaohitaji upasuaji wa dharura.

Polisi na wanajeshi wakiweka ulinzi kwenye moja ya kanisa lililoshambuliwa, 21 Aprili 2019
Polisi na wanajeshi wakiweka ulinzi kwenye moja ya kanisa lililoshambuliwa, 21 Aprili 2019 REUTERS/Dinuka Liyanawatte

Nyaraka iliyoonwa na shirika la habari la Ufaransa AFP iliyoandikwa na mkuu wa polisi Pujuth Jayasundara alitoa onyo siku 10 zilizopita kuwa kuna njama zimepangwa za kutekelezwa kwa mashambulizi yatakayolenga makanisa muhimu nchini humo.

Taarifa hiyo ilionya pia kundi la National Thowheeth Jama'ath lilikuwa limepanga kushambulia makanisa ukiwemo ubalozi wa India mjini Colombo.

Mlipuko wa kwanza uliripotiwa katika kanisa la St Anthony, kanisa ambalo ni maarufu kutembelewa na wageni mjini Colombo, ambapo ilifuatiwa na milipuko mingine iliyolernga hoteli.

Katika hatua nyingine viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May wamekashifu mashambulizi hayo na kuahidi kuisaidia Serikali ya Colombo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.