rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

New Zealand Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Christchurch: Mtuhumiwa akabiliwa na mashitaka 50 ya mauaji

media
Brenton Harrison Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitambuliwa kama mtu mwenye msimamo mkali wa ubaguzi wa rangi, anatuhumiwa kuua watu 50 na kujeruhiwa wengine kadhaa, Machi 15, wakati wa sala ya Ijumaa katika misikiti miwili. REUTERS/Mark Mitchell

Mtuhumiwa wa mauaji katika Misikiti miwili ya Christchurch, nchini New Zealand anakabiliwa na mashitaka 50 ya mauaji na mashitaka thelathini na tisa ya jaribio la mauaji, polisi ya nchi hiyo imesema.


Mashtaka mengine bado yanajadiliwa, polisi imesema katika taarifa yake.

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, ameliita shambulio hilo kama "kitendo cha kigaidi." New Zealand haijawahi kukumbwa na tukio baya la mauaji ya watu wengi kama hilo.

Brenton Harrison Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitambuliwa kama mtu mwenye msimamo mkali wa ubaguzi wa rangi, anatuhumiwa kuua watu 50 na kujeruhiwa wengine kadhaa mnamo Machi 15, wakati wa sala kuu ya Ijumaa katika misikiti miwili huko Christchurch.

Tarrant, ambaye alishtakiwa kwa mauaji wakati aliposikilizwa kwa mara ya kwanza katika mahakama siku moja baada ya shambulio, anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama kuu Ijumaa wiki hii.