rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Indonesia: Waathirika wa tsunami wakabiliwa na njaa na magonjwa

media
Wakazi wakishangilia uharibifu uliosababishwa na tsunami kwenye Pwani ya Carita, Indonesia, Desemba 23, 2018. Antara Foto/Asep Fathulrahman/ via REUTERS

Waokoaji wamekua wakijaribu kutoa misaada kwa mikoa iliyoathirika na Tsunami kufuatia mlipuko wa volkano nchini Indonesia, lakini waliokimbilia katika vituo mbalimbali vya dharura wanaendelea kukabiliwa na uhaba wa maji safi na dawa.


Mashirika ya kihisani yameonya kuhusu hatari za kuibuka kwa magonjwa mbalimbali wakati idadi ya watu waliopoteza maisha ikiendelea kuongeza na kufikiwa mpaka sasa 400.

"Watoto wengi ni wagonjwa, wana homa, wana maumivu kichwani na hawana maji ya kutosha," amesema Rizal Alimin, daktari wa shirika lisilo la kiserikali la Aksi Cepat Tanggap. Siku ya Jumamosi usiku, Tsunami ilipiga visiwa vya Sumatra na Java, na kusababisa vifo vya watu 373, zaidi ya 1,400 kujeruhiwa na 128 kutoweka, kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Idara inayohusika na majanga.

Zaidi ya watu 5,000 wamehamishwa.