rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Tsunami Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Tsunami yauwa watu 168 nchini Indonesia

media
Mlipuko wa Volkano nchini Indonesia Phys.org

Watu zaidi ya 160 wamepoteza maisha na karibu 600 wamejeruhiwa katika mji wa Sunda Strait nchini Insdonesia, baada ya kutokea kwa Tsunami katika mji huo wa Pwani.


Mbali na mauaji hayo, watu zaidi ya 20 bado hawajapatikana lakini pia mamia ya majengo yameharibika.

Maafisa wanasema kuwa, watu wengine zaidi ya 500 wamejeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu.

Kuna hofu kuwa, idadi ya vifo huenda itaendelea kuongezeka.

Watalaam wanasema kuwa chanzo cha janga hilo ni maporomoko ya ardhi, chini ya bahari baada ya kulipuka kwa volkano hivi karibuni.