Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-VIKWAZO

Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran vyaanza kutumika

Serikali ya Iran imesema haitishwi na hatua ya Marekani ya kuiwekea nchi hiyo vikwazo zaidi, kauli inayotolewa wakati huu ambapo utawala wa Washington leo Jumatatu umetangaza vikwazo vipya kwa nchi hiyo.

Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, wakati wa hotuba yake huko Tehran Agosti 13, 2018.
Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, wakati wa hotuba yake huko Tehran Agosti 13, 2018. Official Khamenei website/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili maelfu ya raia wa Iran waliandamana jijini Tehran kukashifu kile ambacho walisema ni vitisho vya Marekani dhidi ya uhuru wa taifa hilo, huku kiongozi wa kidini wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei akisisitiza nchi yake haitatetereka.

Serikali ya Marekani imetangaza kuwa leo Jumatatu itarejesha vikwazo vitakavyolenga sekta ya mafuta na ile ya kifedha, vikwazo ambavyo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema ni vikwazo vigumu zaidi kuwahi kuvichukua.

Vikwazo hivi vinarejeshwa ikiwa ni miezi michache imepita tangu rais Donald Trump afanye uamuzi tata wa kuiondoa nchi yake kwenye mkataba wa nyuklia uliotiwa saini kati ya Iran na mataifa yenye nguvu.

Licha ya kutengwa na Marekani nchi ya Iran inaungwa mkono na mataifa mengi ambayo yamesalia kwenye mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.