Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-VIKWAZO

Iran: Rohani apuuzia mbali vikwazo vipya vya Marekani

Rais wa Iran Hassan Rohani amefutilia mbali vikwazo vipya vya Marekani, akisema kuwa Iran haitotetereka kufuatia vikwazo hivyo. Bw Rohani amelaumu hatua hiyo ya Marekani, akisema ni vita vya kiuchumi vilivyozinduliwa na Washington dhidi ya nchi yake.

Rais wa Iran Hassan Rohani ameonya kwambanchi yake itaenda kuuza mafuta yake, licha ya vikwazo vipya vya MArekani kuanza kutumika, Novemba 5, 2018.
Rais wa Iran Hassan Rohani ameonya kwambanchi yake itaenda kuuza mafuta yake, licha ya vikwazo vipya vya MArekani kuanza kutumika, Novemba 5, 2018. HO / Iranian Presidency / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwenye ukurasa wake wa Twitter Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa mtu yeyote anayeshirikiana kibiashara na Iran kufuatia hatua yake ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya vikwazo vya Marekani kuanza kutumika leo Jumatatu, Rais wa Iran amesema kuwa Iran haitotatizika na vikwazo hivyo vya Marekani

"Tunapuuzia mbali vikwazo hivyo vilivyowekwa kinyume cha sheria na ni kinyume na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kuona Marekani inalazimika kujitenga na nchi nane kwa kununua mafuta ya Iran wakati ilisema wazi kwamba ingepunguza mauzo ya mafuta ya Iran kwa kiwango cha chini kabisa, kwa kweli huu ni ushindi kwetu, " amesea Bw Rohani.

Suala kuu la vikwazo vya Marekani ni mauzo ya mafuta ya Iran, ambayo tayari yameshuka kwa asilimia 30 tangu Marekani kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia mnamo mwezi Mei pamoja na mfululizo wa vikwazo vya Marekani.

Iran inategemea msaada kutoka nchi za Ulaya, Urusi na China ili kukabiliana na vikwazo vya Marekani. Tehran inatarajia kudumisha mauzo ya mafuta kwa kiwango chake cha sasa cha mapipa milioni 1.5 kwa siku. Hii itaiwezesha kuhakikisha uchumi wake unasalia kuwa imara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.