Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANi-BRUNSON-HAKI

Mahakama ya Uturuki yaagiza kuachiliwa huru mchungaji wa Marekani Brunson

Mahakama nchini Uturuki imeagiza Ijumaa wiki hii kuachiliwa huru kwa mchungaji kutoka Marekani Andrew Brunson, ambaye amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi 21. Wadadisi wanasema hatua hii huenda ikachangia kutuliza mvutano kati ya Uturuki na Marekani.

Andrew Brunson (katikati, akinyoosha mkono juu) Izmir Julai 25, 2018.
Andrew Brunson (katikati, akinyoosha mkono juu) Izmir Julai 25, 2018. Demiroren News Agency/DHA via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Andrew Brunson amekuwa akishtumiwa kuwa na uhusiano na wanaharakati wa Kikurdi na wafuasi wa Fetullah Gülen, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Tayyip Recep Erdogan ambaye anaishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1999.

Andrew Brunson, alihukumiwa miaka mitatu na mwezi moja na nusu jela lakini mahakama ya Aliaga, kaskazini mwa Izmir, magharibi mwa Uturuki, ilibaini kwamba alikuwa tayari ametumikia hukumu yake.

Mwanasheria wake, Ismail Cem Halavurt, amesema mchungaji Brunson, ambaye hakuweza kujizuia kuonyesha furaha yake baada ya uamuzi huo, anatarajia kurudi nyumbani nchini Marekani.

Kabla ya hakimu kusema, Andrew Brunson aliiambia mahakama: "Sina hatia, nampenda Yesu, napenda Uturuki."

Kukamatwa na kufungwa kwake kulizua mvutano mkubwa kati ya Washington na Ankara.

Andrew Brunson alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka 35 jela. Ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma iliomba Mchunagji uyo awekwe jela kwa miaka kumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.