Mkutano wa Francophonie waanza Armenia
Viongozi wa Mataifa 84 ya jumuiya ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, Francophonie wanakutana nchini Armenia kujadili mambo mbalimbali lakini pia watamchagua katibu mkuu wa taasisi hiyo.
Imechapishwa:
Waziri wa sasa wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo anayeungwa mkono na Ufaransa anapewa nafasi ya kushinda nafasi hiyo licha ya mkanganyiko kuhusu hatua hiyo ya Ufaransa.
Licha ya Rwanda kulaumiwa kuhusu swala la uhuru wa kujieleza baadhi ya serikali za Francophonie zinaunga mkono mgombea wake huku Canada na Quebec ambazo awali zilionekana kumunga mkono Michael Jean zimetangaza kutomuunga mkono mgombea huyo raia wa Canada
Kawaida nafasi hiyo viongozi wa nchi wanachama huteuwa baada ya wagombea kuachiana nafasi, lakini Michael Jean amekataa kuachia nafasi na kutaka mchuano.