rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ukraine

Imechapishwa • Imehaririwa

Maelfu ya watu wahamishwa kufuatia milipuko katika ghala la silaha Ukraine

media
Visa kadhaa vya moto vilitokea katika ghala za silaha na vifaa vingine vya kivita katika miaka ya hivi karibuni nchini Ukraine. REUTERS/Valentyn Ogirenko

Maelfu ya watu wamehamishwa mapema Jumanne asubuhi kufuatia kisa cha moto na milipuko katika ghala linalomilikiwa na Wizara ya Ulinzi, kilomita 180 mashariki mwa mji mkuu wa Ukraine, Kiev, kwa mujibu chanzo cha kijeshi.


Serikali ya Ukraine haijasema kuhusu hasara iliyotokea na haijulikani kwa wakati huu kama tukio hili ni ajali la kawaida au ni shambulizi.

Hakuna ndege yeyote au helikopta inayorihusiwa kupaa juu ya anga ya eneo hilo la tukio na safari za reli zimesitishwa katika eneo hilo.

Visa kadhaa vya moto vilitokea katika ghala za silaha na vifaa vingine vya kivita katika miaka ya hivi karibuni nchini Ukraine.