rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Idadi ya watu waliopoteza maisha yafikia 1,411, Indonesia

media
Wanajeshi wakimuhudumia mtu aliyejeruhiwa katika uwanja wa ndege wa Palu Oktoba 2, 2018. RFI/Bertrand Haeckler

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi na Tsunami katika Kisiwa cha Celebes nchini Indonesia imepanda na kufikia zaidi ya 1,400 Jumatano wiki hii.


Hata hivyo mambo mengi yanahitajika katika maeneo ya yaliyoathirika na zoezi la kutafuta miili ya watu waliofariki na manusura waliokwama chini ya vifusi vya nyumba linaendelea.

"Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Indonesia imefikia 1,411 Jumatao wiki hii, amesema Tohir, msemaji wa jeshi. Idara inayokabiliana na majanga ya asili imebaini kwamba tayari miili 519 imezikwa.

Mamlaka imetoa muda hadi Ijumaa, wiki moja baada ya kutokea tukio hilo, ili kuwapata watu ambao inawezekana kuwa wamenusurika.

Watu 1,600 walihamishwa kupitia bahari na meli ya kijeshi ya Indonesia ambayo iliweza kuegesha, ikiwa ilibeba misaada ya kibinadamu, katika mji wa pwani wa Palu.