rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Idadi ya vifo yaendelea kuongezeka indonesia kufuatia tetemeko la ardhi

media
Hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Indonesia baada ya maeneo kadhaa kukumbwa na tetemeko la ardhi na tsunami. REUTERS/Beawiharta

Miili ya wanafunzi 34 nchini Indonesia imepatikana chini ya Kanisa liliporomoka jijini Palu. Tetemeko la ardhi lilipiga baadhi ya maeneo ya nchi hiyo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata 6.


Hii inafikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, kufikia zaidi ya 1,234 kwa mujibu wa takwimu iliyotolewa hivi leo.

Maafisa nchini humo wanasema bado wanaendelea kutafuta miili zaidi au manusura, na idadi ya watu waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka.

Hata hivyo, juhudi za kutafuta miili zaidi inakwamishwa na miundo mbinu mibaya,kwa sababu maeneo mengi yameharibiwa nchini humo.

Shughuli za kawaida zimekwama nchini humo, watu hawana furaha, wakati huu serikali ikitoa wito kwa wahisani kutoka maeneo mbalimbali duniani kujitokeza kuwasaidia raia wa nchi hiyo.

Watu walioponea tetemeko hilo wanahitaji dawa, chakula na makaazi ili kuepusha vifo zaidi vinavyoweza kusababishwa na hali inayoshuhudiwa.