Pata taarifa kuu
MALDIVES-SIASA

Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguzi Maldives

Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Maldives yanaonesha kuwa kinara wa upinzani Ibrahim Mohamed Solih ameshinda nafasi hiyo, matokeo ambayo ni mshtuko kwa rais Abdulla Yameen ambaye waangalizi wengi walimtuhumu kwa kujipendelea wakati wa kampeni.

Kiongozi wa upinzani nchini MAldives, Ibrahim Mohamed Solih, Septemba 23, 2018.
Kiongozi wa upinzani nchini MAldives, Ibrahim Mohamed Solih, Septemba 23, 2018. REUTERS/Ashwa Faheem
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, Solih amepata asilimia 58.3 ya kura zote.

Shangwe zilishuhudiwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, huku Solih mwenyewe akiahidi kuwa rais wa wananchi wote na kuleta mabadiliko kwenye taifa hilo ambalo mara kadhaa limeshuhudia sintofahamu ya kisiasa.

Uchaguzi wa safari hii umefanyika huku mamia ya wanasiasa wa upinzani na wakosoaji wa Serikali wakiwa jela au nje ya nchi walikokimbilia kuomba hifadhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.