rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Majanga ya Asili Joko Widodo

Imechapishwa • Imehaririwa

Tetemeko la ardhi Lombok: Watu zaidi 430 wapoteza maisha

media
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi Lombok, Indonesia, imeongezeka na kufikia zaidi ya 430. REUTERS/ Antara Foto/Ahmad Subaidi

Tetemeko la ardhi lililopiga kisiwa cha Lombok nchini Indonesia Agosti 5 imesababisha watu zaidi ya 430 kupoteza maisha. Shughuli ya kutafuta watu walioffunikwa na udongo au kukwama chini ya vifusi linaendelea.


Tetemeko hilo la ardhi pia limesababisha uharibifu wa vitu na mali vyenye thamani ya dola milioni 350i, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu wiki hii na taasisi inayokabiliana na Majanga nchini humo (BNPB).

Zaidi ya watu 350,000 walilazimika kuyahama makaazi yao kwa wakati mmoja.

"Uharibifu na hasara ni kubwa," amesema Sutopo Nugroho, msemaji wa taasisi inayokabiliana na Majanga (BNPB).

Jumatatu wki hii rais wa Indonesia Joko Widodo amezuru maeneo yaliyokumbwa na tukio hilo.

Ameomba kuimarisha shughuli za upelelezi na uokoaji, kwa kuzingatia maeneo ambako wanaweza kupatikana watu waliotoweka.