Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-VATICAN-PAPA FRANCIS-HAKI

Papa akubali kujiuzulu kwa askofu mkuu aliyehukumiwa Australia

Papa Francis amekubali kujiuzulu kwa askofu mkuu wa Australia aliyehukumiwa mwaka mmoja jela kwa kushindwa kufichua vitendovya udhalilishaji watoto kingono vilivyoendeshwa na viongozi wa kidini nchini humo, ofisi ya Papa Francis imesema katika taarifa yake.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis.
Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis. REUTERS/Stefano Rellandini
Matangazo ya kibiashara

"Papa Francis amekubali kujiuzulu kwa Askofu Mkuu wa Adelaide (Australia) Philip Edward Wilson," taarifa hiyo imeongeza.

 

ASKOFU Mkuu wa jimbo la Adelaide nchini Australia, Philip Edward Wilson, ambaye ni afisa mwandamizi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani alikutwa Mei 2018 na hatia ya kuficha unyanyasaji watoto kingono na hivyo kuhukumiwa kifungo kisichopungua miezi 12 jela na kisichozidi miaka miwili.

Makosa yake ni kufunika uhalifu wa kuhani Jim Fletcher ambaye katika miaka ya 1970 aliwadhalilisha kingono watoto katika eneo la Hunter, New South Wales.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Newcastle Robert Stone alimhukumu Wilson miezi 12 ya kufungwa kwa muda bila kuwa huru kwa miezi sita.

“Mtuhumiwa hakuonyesha huruma hata kidogo. Kwa maoni yangu hukumu haipaswi kusitishwa.

Stone pia aliamuru kuwa Wilson afanyiwe tathmini kwa kizuizi cha nyumbani; kumaanisha kuwa anaweza kuepuka jela. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 14.

Uchunguzi wa Miaka mitano na Tume ya Royal juu ya unyanyasaji wa kijinsia wa watoto ulipata kua mwaka jana makumi ya maelfu ya watoto walifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia kati ya 1960 na 2015 katika taasisi za Australia, ikiwa ni pamoja na shule na makanisa.

Pia iligundulika kuwa asilimia 7 ya makuhani wote kati ya ,mwaka 1960 na 2015 walidaiwa kuwadhulumu watoto na asilimia 62 ya waathirika, ambao waliripoti unyanyasaji katika taasisi ya kidini, walikuwa kutoka kwa taasisi zilizosimamiwa na kanisa Katoliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.