Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-MAREKANI-USALAMA

Seoul yathibitisha kusitishwa kwa mazoezi yake ya kijeshi na Marekani

Korea Kusini imethibitisha Jumanne wiki hii kwamba mazoezi yake ya kijeshi ambayo yangelifanyika mnamo mwezi Agosti na Marekani yamefutwa mwaka huu, lakini imesema itaandaa mazoezi yake yenyewe.

Korea Kusini inasema itaendelea na mazoezi yake ya kishehi.
Korea Kusini inasema itaendelea na mazoezi yake ya kishehi. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Usalama na Ulinzi wametoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari.

Seoul na Washington walitangaza mwezi Juni kuwa wamesitisha mazoezi yao ya pamoja ya kijeshi ya Ulchi Freedom Guardian ili kuheshimu ahadi iliyotolewa na rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano wake wa Juni 12 huko Singapore na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ya kusitisha "michezo ya vita".

Ofisi ya rais wa Korea Kusini imebaini kwamba kusimamishwa kwa mazoezi haya ya pamoja ya kijeshi kunaweza kuwezesha mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

Kwa upande wake, Korea Kusini imesema itaendeleza mfumo mpya wa mazoezi yake ya kijeshi kwa kuunganisha Ulchi na mazoezi yake mengine ya Taeguk. Mfumo huu mpya unalenga kuzuia mashambulizi na majanga ya asili kwa kiasi kikubwa, mawaziri wa Usalama na Ilinzi wa Korea Kusini wamesema.

Mawaziri hao wameongeza kuwa mazoezi hayo ya Korea Kusini yatazinduliwa mnamo mwezi Oktoba wakati wa mazoezi ya kawaida kwenye uwanja wa Hoguk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.