rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Bunge la Uingereza latarajia kupiga kura mkataba wa kujitoa EU kabla ya Januari 21 (Downing Street)

China Ujerumani

Imechapishwa • Imehaririwa

China yamruhusu mke wa mwanaharakati Liu Xiaobo kuondoka

media
Mjane wa Liu Xiaobo aliyefariki dunia kutokana na saratani ya ini wakati akitumikia kifungo cha mikaa 11 ameruhusiwa kuondoa nchini China. REUTERS

Liu Xia, mjane wa Liu Xiaobo, ambaye alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2010, ameondoka Beijing mapema Jumanne wiki hii na anaelekea mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, mmoja wa marafiki zake, mwandishi Ye Du, amethibitisha taarifa hiyo kwa shirika la habari la Reuters.


Kuondoka kwa Liu Xia, ambaye amesafiri kwa ndege ya Finnair kwenda Helsinki saa 11:00 asubuhi (sawa na 01:00 saa za Afrika ya Kati), kunakuja baada ya miezi kadhaa mashirika ya haki za binadamu yakipambana kwa kuishinikiza serikali ya China kuruhusu mshairi huyo kuondoka nchini.

Jumanne wiki hii, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amekamilisha ziara yake nchini Ujerumani, nchi ambayo kwa muda mrefu imekua ikiomba, kwa mujibu wa wanadiplomasia wa Magharibi, Liu Xia kuondoka nchini China.

Liu Xiaobo, mwandishi, profesa wa chuo kikuu na mwanaharakati wa haki za binadamu nchini China, alifariki dunia kutokana na saratani ya ini mnamo Julai 13, 2017, wakati alipokua akitumikia kifungo cha miaka 11 kwa kosa la "uasi" mwaka 2009 .

Miezi michache baada ya kifo cha mumewe, Liu Xia alipewa kifungo cha nyumbani tangu 2010. Mamlaka ya China imehakikisha kuwa yuko huru na anaruhusiwa kutekeleza haki zake zote.

Liu Xia "ataanza maisha mapya" huko Ulaya, ameandika kwenye ujumbe wa WeChat ndugu yake mdogo, Liu Hui. Liu Hui alihukumiwa mwaka 2013 na mahakama ya China kwa kosa la "udanganyifu". Lakini yuko huru chini ya uangalizi wa mahakam, kwa mujibu wa ndugu zake.

Ubalozi wa Ujerumani huko Beijing haukuweza kuthibitisha taarifa hii.